• HABARI MPYA

    Friday, May 06, 2016

    AZAM HATA WAKIFUNGWA NA YANGA WATACHEZA TU MICHUANO YA AFRIKA

    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kwamba iwapo Bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu 2015/16 inayoendelea atashinda pia taji katika fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ndiye atayeiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya mabingwa wa Afrika msimu wa 2016/17.
    TFF imesema kwa mantiki hiyo, timu ambayo itafungwa katika fainali ya Kombe la ASFC inayodhaminiwa na kituo cha Televisheni cha Azam, ndiyo itakayowakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika katika msimu wa 2016/17.

    Fainali za Kombe la Shirikisho zinatarajiwa kufanyika baadaye mwezi ujao, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mchuano uliohusisha timu 64 za Ligi Kuu Tanzania Bara - VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL (24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).
    Yanga na Azam FC zimeingia Kombe la AFC wakati katika Ligi Kuu zinachuana na SImba SC kuwania ubingwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM HATA WAKIFUNGWA NA YANGA WATACHEZA TU MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top