• HABARI MPYA

    Saturday, May 21, 2016

    AIRTEL RISING STARS NA TFF WAPANGA MIKAKATI YA KUINUA SOKA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya Airtel Tanzania jana Ijumaa Mei 20, 2016 imekutana na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kuzungumzia mipango ya maendeleo wa mpira wa miguu nchini ikiwa ni pamoja na michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza Juni mwaka huu.
    Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine ambaye ndio aliongoza kikao hicho, alitoa shukrani ka kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la vijana ambalo ndio msingi wa kukuza mpira wa miguu nchini. “Naamini ya kwamba kwa kuendelea kuwekeza kwenye soka la vijana, tutaweza kufika mbali kwa kupata matokeo mazuri.”
    Tangu kuanzisha kwa michuano ya Airtel Rising Stars miaka mitano iliyopita, soka la vijana nchini imekuwa na mafanikio makubwa“Leo, Timu ya Taifa chini ya miaka 20 – Serengeti Boys, imeundwa na vijana ambao wamekuwa ni chimbuko la Airtel Rising Stars,” alisema Selestine na kuongeza kuwa hata timu ya Taifa ya Wanawake – Twiga Stars, Klabu za Liguu na zile zinazoshiriki ligi daraja ya kwanza, zinatumia wachezaji ambao wamekuzwa kwa michuano ya Airtel Rising Stars.
    Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa (kulia)

    Airtel imeweza kuiwezesha TFF kufika maeneo ambayo yamekuwa ni vigumu kufika kutafuta vipaji. Kwa kufanya hivyo, tuweza kupata vijana wenye vipaji vingi na hata kwa sasa hivi, baadhi yao wako na Timu ya Taifa ya Vijana Serengeti kushiriki michuano ya Kimataifa inayoendelea India, alisema Mwesigwa.
    Katibu Mkuu huyo wa TFF aliomba Airtel kuendelea kudhamini miradi ya soka ya vijana kwa vile ndio njia pekee Tanzania inaweza kuwa na timu bora na imara ya Taifa. Nchi nyingi zinazofanya vizuri kwenye michuano mbali mbali ya soka ni kwa vile waliweza kuwekeza kwenye program mbali mbali za vijana kama vile Airtel Rising Stars. Kwa kushirikiana na nyinyi, tutaweza kupata na kukuza vipaja vya soka ambazo watakuwa na msaada mkubwa kwenye timu ya Taifa.
    Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema “kampuni yake itaendelea kudhamini program za soka la vijana ambazo zimeweza kuwa na mafanikio makubwa kwa miaka mitano iliyopita. Lengo letu ni kuwa na timu ya taifa bora kama vile Misri, Cameron, Nigeria, Ivory Coast na Ghana,” alisema Mmbando huku akisisitiza njia pekee ya kufikia mafanikio hayo ni kuwekeza na kukuza soka la vijana.
    Airtel pia imetoa shukrani kwa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Michezo na Sanaa pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushirikiano wao ambao umeifanya Airtel Rising Stars kuwa moja ya mashindano yenye mafanikio makubwa hapa Tanzania. Bila ushirikiano na serikali pamoja na wadau wa soka hapa nchini, Airtel Rising Stars hangeweza kufika hapa ilipo kwa leo, alisema Mmbando.
    Mmbando alisema kwa mwaka huu, Tanzania haitashiriki kwenye michuano ya kimataifa ambayo huleta pamoja wachezaji waliong’ara kwenye nchi zao Barani Afrika kwa ajili ya kubadilisha uzoefu, bali itashirikiana na TFF kuweka mikakati  mingi zaidi ya kuwawezesha vijana hawa kufanya vyema hata baada ya mashindano ya Airtel Rising Stars kwisha.
    Tayari Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi amepanga ratiba kamili ya michuano hiyo kwa mwaka huu ambako kwa sasa inajadiliwa na itatoa wakati wowote wiki ijayo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AIRTEL RISING STARS NA TFF WAPANGA MIKAKATI YA KUINUA SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top