• HABARI MPYA

    Friday, April 15, 2016

    SIMBA NA TOTO LA YANGA JUMAPILI TAIFA

    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.
    Jumamosi, Yanga watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Ndanda FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Nang’wanda Sijaona mjini Mtwara.
    Coastal Union watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Mkwakwani jinini Tanga, huku Jumapili, Simba SC wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA TOTO LA YANGA JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top