• HABARI MPYA

  Sunday, April 17, 2016

  NIYONZIMA: TUNAKWENDA KULIPA KISASI KWA AL AHLY

  Na Somoe Ng'itu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Yanga kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima (pichani kulia) amesema kwamba aliumia kuukosa mchezo wa kwanza wa mashindano ya Klabu Bingwa dhidi ya Al Ahly ya Misri ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.
  Akizungumza na gazeti hili jana, Niyonzima alisema kwamba anaamini atakaporejea kwenye kikosi hicho, ataisaidia timu na hatimaye kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
  Niyonzima alisema kwamba kila mchezaji wa Yanga amejipanga kujituma ili kulipiza kisasi kwa Waarabu hao ambao waliwafunga kwa penalti 4-3 walipokutana kwenye michuano hiyo mwaka juzi.
  "Namshukuru Mungu nimepona, nilikuwa na malaria 5, ila sasa niko vizuri na mazoezi pia nimeshaanza, kiukweli niliuimia sana kukaa jukwaani katika mechi ile ya Jumamosi," alisema kiungo huyo wa zamani wa APR ya Rwanda.
  Yanga inatarajia kusafiri leo Jumapili saa 10 jioni kuelekea Alexandria kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika Aprili 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIYONZIMA: TUNAKWENDA KULIPA KISASI KWA AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top