• HABARI MPYA

    Friday, April 15, 2016

    MALINZI 'AMPA GWALA' RAVIA KUTETEA UKUU ZFA

    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (pichani kushoto) amempongeza Ravia Idarous Faina wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi ulifanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Gombani, Pemba.
    Katika salamu zake, Malinzi amesema anampongeza Ravia kwa kuchaguliwa kwake, na hiyo imeonyesha imani kubwa kwa waliomchagua kuongoza ZFA katika kipindi kingine.
    Malinzi amewapongeza vingozi wote wapya waliochaguliwa katika uchaguzi huo, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika shughuli zote za maendeleo ya mpira wa miguu.
    Uchaguzi wa kupata viongozi wa ZFA ulifanyika jana Gombani kisiwani Pemba, ambapo Ravia aliibuka mshindi na kutetea nafasi yake, nafasi ya makamu wa rais Ugunja kienda kwa Mzee Zam Ali, na makamu wa Pemba ikichukuliwa na Ali Mohamed Ali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI 'AMPA GWALA' RAVIA KUTETEA UKUU ZFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top