• HABARI MPYA

  Saturday, April 16, 2016

  KIPRE TCHETCHE, SERGE WAWA WOTE HAWAENDI TUNISIA, TATIZO MISULI

  Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kati wa Azam FC, Serge Wawa Pascal na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche, wote raia wa Ivory Coast hawatasafiri na timu kwenda Tunisia kesho.
  Wawili hao wote watakosekana kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance Jumatano mjini Tunis kutokana na kuwa majeruhi. 
  Daktari Msaidizi wa Azam FC, Talib Omar ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE  leo kwamba Wawa aliumia misuli katika mechi ya kwanza dhidi ya Esperance Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Azam ikishinda 2-1.
  Kipre Tchetche hatasafiri na timu kwenda Tunisia kesho kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli  

  Dk. Omar amesema jithada za kumrejesha mapema uwanjani Wawa zimeshindikana na sasa ataendelea na matibabu na hatasafiri na timu kwenda Tunisia.
  Dk. Omar amesema kwamba Kipre naye aliumia Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Azam ikishinda 1-0.
  “Kipre naye ameumia misuli pia, kwa hiyo wachezaji hao pamoja na beki wetu mwingine tegemeo, Shomary (Kapombe) ambaye ni mgonjwa wote watakosekana katika mchezo huo,”amesema Dk. Omar.
  Lakini Dk. Omar amesema kwamba habari njema ni kwamba kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyekuwa majeruhi hadi akaukosa mchezo wa kwanza na Esperance amepona na anatarajiwa kusafiri na timu.
  Azam inaondoka kesho kwenda Tunisia ikihitaji kuulinda ushindi wake wa 2-1 nyumbani ili kuingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPRE TCHETCHE, SERGE WAWA WOTE HAWAENDI TUNISIA, TATIZO MISULI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top