• HABARI MPYA

    Sunday, February 14, 2016

    YANGA SC WAWASILI PEMBA KWA KAMBI YA 'KUUWA MNYAMA' JUMAMOSI TAIFA

    Wachezaji wa Yanga SC, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar tayari kuunganisha ndege kwenda Pemba kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba SC Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
    Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro tayari kikosi cha Yanga SC kipo Pemba na kesho kitaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani
    Yanga SC iliondoka Dar es Salaam Ijumaa Saa 1:00 usiku kwenda Mauritius kabla ya leo kutuan Zanzibar
    Yanga SC iliwasili Zanzibar majira ya Saa 4:00 asubuhi na hadi Saa 6:00 mchana, tayari walikuwa Pemba
    Yanga SC jana ilishinda 1-0, Mauritius, bao pekee la Mzimbabwe Donald Ngoma dhidi ya wenyeji Cercle de Joachim katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika na timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo Dar es Salaam

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAWASILI PEMBA KWA KAMBI YA 'KUUWA MNYAMA' JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top