• HABARI MPYA

    Friday, February 05, 2016

    YANGA SC KUONDOKA JUMATANO DAR KUIFUATA JOACHIM CERCLE DE UFUNGUZI LIGI YA MABINGWA AFRIKA 2016

    RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
    Februari 6, 2016
    African Sports Vs Stand United
    Februari 7, 2016
    Kagera Sugar Vs Simba SC
    Mbeya City Vs Prisons
    JKT Ruvu Vs Yanga SC
    Ndanda FC Vs Mtibwa Sugar
    Azam FC Vs Mwadui FC
    Toto Africans Vs Coastal Union
    Majimaji Vs Mgambo JKT
    Yanga SC wanaanza kazi Ligi ya Mabingwa Afrika wiki ijayo

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    YANGA SC itacheza na JKT Ruvu Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kabla ya kupanda ndege Jumatano, kwenda Mauritius kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Cercle de Joachim.
    BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE inafahamu maandalizi ya safari yanaendelea na mpango ni timu iondoke Jumatano, ikiwa ni siku tatu kabla ya mchezo ili kuzoea hali ya hewa.
    Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm baada ya kuwafanyia tathmini ya kina Joachim anaamini aina ya maanedalizi yake kabla ya mchezo wa Jumamosi ya wiki ijayo, yatatosha kabisa kufanya vizuri katika mechi ya kwanza iliyopangwa kuanza Saa 9:30 Alasiri kwa saa za Mauritius Uwanja wa Curepipe mjini Curepipe.
    Kwa ujumla, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho na keshokutwa nchini.
    Kesho kutakuwa na mchezo mmoja tu Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kati ya wenyeji African Sports na Stand United ya Shinyanga.
    Jumapili, mbali na Yanga SC kumenyana na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam – Kagera Sugar watawakaribisha Simba SC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga wakati Azam FC watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Uwanja wa Sokoine, Mbeya, kutakuwa na mechi ya mahasimu wa Jiji, Mbeya City dhidi ya Prisons, wakati Ndanda FC wataikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Toto Africans wataikaribisha Coastal Union Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Majimaji watakuwa wenyeji wa Mgambo JKT Uwanja wa Majimaji, Songea.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC KUONDOKA JUMATANO DAR KUIFUATA JOACHIM CERCLE DE UFUNGUZI LIGI YA MABINGWA AFRIKA 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top