• HABARI MPYA

  Sunday, February 14, 2016

  VIBONDE WA AZAM FC WAITWANGA MAMELODI 1-0 LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  TIMU ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini jana imemaliza wimbi lake la kucheza mechi 19 bila kufungwa, baada ya kuchapwa bao 1-0 na Chicken Inn katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa nchini Zimbabwe jana.
  'Wabrazil' hao mara ya mwisho walifungwa Septemba mwaka jana, lakini bao pekee la Mitchell Katsvairo dakika ya 39 jana liliwaondoa vichwa chini.
  Chicken Inn wameifunga 1-0 jana Mamelodi Sundowns katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika

  Kocha Pitso Mosimane alifanya mabadiliko mawili tu kutoka kikosi kilichoshinda dhidi ya Orlando Pirates katika Ligi ya nyumbani katikati ya wiki akimuondoa langoni kipa Denis Onyango, wakati Themba Zwane alichukua nafasi ya Khama Billiat, aliyeripotiwa kuumia wakati wa mazoezi ya kabla ya mchezo wa jana.
  Sundowns watawakaribisha Chicken Inn iliofungwa na Azam FC mabao 3-1 katika michuano maalum Zambia wiki mbili zilizopita, Februari 27, mwaka huu katika mchezo wa marudiano wakishinda ushindi wa kuanzia mabao 2-0 ili kusonga mbele.
  Timu hiyo ya Pretoria ilishika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu uliopita na pia ikatwaa Kombe la Nedbank, baada ya kuwafunga Ajax Cape Town.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VIBONDE WA AZAM FC WAITWANGA MAMELODI 1-0 LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top