• HABARI MPYA

  Saturday, February 13, 2016

  TIMU YA MATOLA YAUA 8-0 NA KUPANDA LIGI KUU, TFF ‘YAFUTA’ MATOKEO

  Kocha wa Geita, Suleiman Matola
  TIMU ya Geita Gold ya Geita imeshinda mabao 8-0 dhidi ya JKT Kanembwa katika mchezo wa mwisho wa Kundi C Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, hivyo kujihakikishia kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Hiyo inafuatia waliokuwa wapinzani wao, Polisi Tabora kushindi mabao 7-0 dhidi ya JKT Oljoro katika mchezo mwingine wa mwisho wa kundi hilo leo.
  Matokeo hayo yanazifanya timu zote zimalize na pointi 33 baada ya michezo yote 15, lakini Geita inayofundishwa na Suleiman Matola inaongoza kundi hilo kwa wastani mabao, ikiwa na wastani (GD) wa mabao 23 dhidi ya 22 ya Polisi.
  Hata hivyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema halitatangaza timu iliyopanda Ligi Kuu kutoka Kundi C, hadi itakapoamuliwa na vyombo husika.
  TFF imefikia hatua hiyo ili kupata nafasi ya kupitia taarifa za michezo kati ya JKT Kanembwa dhidi ya Geita Gold na Polisi Tabora dhidi ya JKT Oljoro iliyochezwa leo jioni katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
  “Taarifa za michezo hiyo kutoka kwa wasimamizi husika na vyanzo vingine vinakusanywa ili zifanyiwe kazi na vyombo husika vya TFF,”imesema taarifa ya TFF kwa BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jioni ya leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA MATOLA YAUA 8-0 NA KUPANDA LIGI KUU, TFF ‘YAFUTA’ MATOKEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top