• HABARI MPYA

  Monday, February 15, 2016

  TIMU YA KWANZA YA MBWANA SAMATTA YAPANDA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAN
  TIMU ya kwanza Mbwana Ally Samatta kuchezea katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, African Lyon imepanda tena katika ligi hiyo.
  Lyon imepanda kutoka Kundi A, ikizipiku KMC, Ashanti United na Friends Rangers, zote za Dar es Salaam. Lyon imemaliza na pointi 27 baada ya mechi zote 14, ikifuatiwa na KMC pointi 25, Ashanti United 24 na Rangers 23 sawa na Kilivya United.  
  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeipongeza, Lyon FC ambayo zamani ilikuwa inajulikana kama Mbagala Market kwa kufanikiwa kurejea Ligi Kuu.
  African Lyon ndiyo timu iliyomtoa Mbwana Samatta

  African Lyon imeungana na timu ya Ruvu Shooting FC ya Mlandizi mkoa wa Pwani iliyokua timu ya kwanza kupanda ligi kuu wiki iliyopita kutoka kundi B, wakati Kundi C TFF bado haijaamua licha ya matokeo ya mwishoni mwa wiki Geita Gold kufungana kwa pointi na wastani wa bao ya kufunga na kufungwa (GD)  na Polisi Tabora.
  Baada ya kufanya vizuri akiwa na African Lyon, Samatta alisajiliwa Simba SC mwaka 2010 na mwaka 2011 akahamia TP Mazembe ya DRC, iliyomuuza KRC Genk ya Ubelgiji Januari. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA KWANZA YA MBWANA SAMATTA YAPANDA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top