• HABARI MPYA

  Saturday, February 13, 2016

  SIMBA SC WAHAMA ZANZIBAR KAMBI DHIDI YA YANGA, SASA MAMBO MORO

  KLABU ya Simba SC, inatarajiwa kwenda Morogoro kesho kuweka kambi kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Yanga SC utakaofanyika Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Simba itatua Moro 'Mji Kasoro Bahari' kesho ikitokea mkoani Shinyanga ambako leo itamenyana na Stand United katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu - na hiyo ni tofauti na mazoezi ya klabu kuweka kambi Zanzibar kabla ya mchezo mahasimu wao hao.
  Yanga SC ambayo ipo Mauritius ambako leo watamenyana na , baada ya mchezo watapanda ndege ya Shirika la Tanzania (ATC) kwenda kambi kisiwani Pemba.
  Ikumbukwe mechi ya mzunguko wa kwanza Simba ililala  2-0, mabao ya Malimi Busungu na Amissi Tambwe.
  Hata hivyo, Febaruri 20, Simba SC wataingia Uwanja wa Taifa na kocha mwingine, Mganda Jackson Mayanja aliyeichukua timu mwezi uliopita baada ya kufukuzwa Muingereza, Dylan Kerr ambaye Yanga ilimfunga 2-0 mwaka jana. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAHAMA ZANZIBAR KAMBI DHIDI YA YANGA, SASA MAMBO MORO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top