• HABARI MPYA

  Monday, February 01, 2016

  PELLEGRINI NJE MAN CITY, GUARDIOLA NDIYE KOCHA MPYA ETIHAD

  KOCHA Pep Guardiola amesaini Mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Manchester City baada ya kuthibitishwa Manuel Pellegrini ataondoka Etihad mwishoni mwa msimu.
  Pellegrini alifichua habari hizo katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo kuelekea mchezo dhidi ya Sunderland kesho, wakati City imesema imekuwa ikimuhitaji Guardiola tangu mwaka 2012.
  City imekuwa ikiendesha kwa siri mipango ya kumchukua kocha impendaye, Guardiola kabla ya leo kuweka wazi atajiunga na timu.
  Pep Guardiola amesaini Mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Manchester City msimu ujao

  MATAJI ALIYOSHINDA PEP GUARDIOLA 

  BARCELONA:
  La Liga: 2008–09, 2009–10, 2010–11
  Copa del Rey: 2008–09, 2011–12
  Supercopa de España: 2009, 2010, 2011
  Ligi ya Mabingwa ya UEFA: 2008–09, 2010–11
  Super Cup ya UEFA: 2009, 2011
  Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA: 2009, 2011
  BAYERN MUNICH: 
  Bundesliga: 2013–14, 2014–15
  DFB-Pokal: 2013–14
  Super Cup ya UEFA: 2013
  Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA: 2013
  Pellegrini amesema klabu haitaendelea naye baada ya kumakliza msimu na tayari kocha mpya amepatikana.
  Taarifa ya Man City imesema; "Manchester City inaweza kuthibitisha kwamba katika wiki za karibuni imekuwa ikishughulikia kukamilisha Mkataba na Pep Guardiola awe kocha Mkuu wa MCFC kwa msimu wa 2016/17 wa Ligi Kuu ya England kuendelea.
  "Mkataba ni wa miaka mitatu. Majadiliano hayo ni matokeo mijadala ya mwaka 2012. Kwa heshima yetu kwa Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu inataka kuweka wazi uamuzi wake kwa jamii ili kuzuia tetesi zisizo za kawaida. 
  Sasa Pellegrini ataendelea na kazi Manchester City hadi mwishoni mwa msimu kabla ya kumpisha kocha mpya, Guardiola ambaye kwa sasa anafundisha Bayern Munich ya Ujerumani iliyomchukua kutoka Barcelona ya Hispania. 

  Manuel Pellegrini amethibitisha ataondoka Manchester City mwishoni mwa msimu kumpisha Guardiola
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PELLEGRINI NJE MAN CITY, GUARDIOLA NDIYE KOCHA MPYA ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top