• HABARI MPYA

  Wednesday, February 03, 2016

  NI DRC AU GUINEA KUTANGULIA FAINALI? KESHO NI MALI NA IVORY COAST

  NUSU Fainali ya kwanza ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, inatarajiwa kuchezwa leo.
  Mabingwa wa kwanza wa CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanatarajiwa kumenyana na 
  Guinea Uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Rwanda kuanzia Saa 10:00 jioni.
  Furaha hii itaendelea kwa wachezaji wa DRC leo?

  DRC iliwatoa wenyeji, Rwanda katika Robo Fainali kwa kuwachapa mabao 2-1 baada ya dakika 120, wakati Guinea iliwatoa Zambia kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Umuganda. Gisenyi.
  Nusu Fainali ya pili inatarajiwa kufanyika kesho, ikizikutanisha timu za Afrika Magharibi tupu, 
  Mali na Ivory Coast Uwanja wa Nyamirambo kuanzia Saa 10:00 pia.
  Mali iliwastaajabisha wengi kwa kuwatoa mabingwa wa mwaka 2011, Tunisia kwa kuwachapa mabao 2-1, wakati Ivory Coast iliwatoa Cameroon kuwa kuwatandika mabao 3-0.
  Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu wa michuano hiyo ya nne, baada ya iIe ya 2009 Ivory Coast, 2011 Sudan na 2014 Afrika Kusini ambako Libya waliibuka mabingwa, zitafanyika Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI DRC AU GUINEA KUTANGULIA FAINALI? KESHO NI MALI NA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top