• HABARI MPYA

  Saturday, February 13, 2016

  NGASSA ATOKEA BENCHI, FREE STATE YAPIGWA 1-0 NA COSMOS

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa (pichani kushoto) ametokea benchi jana kipindi cha pili, lakini akashindwa kuinusuru timu yake, Free State Stars kulala 1-0 mbele ya Jomo Cosmos katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini jioni ya leo Uwanja wa Olen Park mjini Potchefstroom.
  Ngassa aliingia dakika ya 81 kuchukua nafasi ya Danny Venter, lakini wakati huo tayari wenyeji Jomo Cosmos wamekwishapata bao lao pekee la ushindi lililofungwa na Cheslyn Jampies dakika ya 53.
  Kikois cha Cosmos kilikuwa: Naicker - Nsabiyumva, Mthembu, S Khumalo, Machupu - Lingwati, Jampies, Zulu/Maluleke dk86, Mashumba/Nomandela dk89, Aka/Madolo dk69 na Makobela.
  Free State Stars: Diakite, Mashego, Sankara, Kerspuy, Mbhele/A Nkosi dk64, Venter/Ngassa dk81, Masehe, Makhaula, Gopane, Mohomi na Somaeb/Japhta dk73.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA ATOKEA BENCHI, FREE STATE YAPIGWA 1-0 NA COSMOS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top