• HABARI MPYA

    Saturday, February 13, 2016

    MVUA YATISHIA AMANI PAMBANO LA YANGA SC NA CERCLE JOACHIM

    MECHI ya kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji, Cercle de Joachim dhidi ya Yanga SC iko shakani kufanyika kutokana na tishio la mvua.
    Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 9:30 Alasiri kwa saa za Mauritius Uwanja wa Curepipe mjini Curepipe, yaani saa moja zaidi kwa saa za Dar es Salaam.
    Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga aliyembatana na timu timu mjini Curepipe, amesema Uwanja una maji, lakini mpira unaweza kuchezeka.
    “Tunasubiri busara ya waamuzi, wakiona mpira utachezeka, sawa. Kwa sasa timu zinapasha kwa ajili ya kuanza mechi,”amesema Sanga.
    Beki wa kushoto Haji Mwinyi anaanzia benchi wakati nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' amepumzishwa na nahodha wa mchezo wa leo anakuwa ni Haruna Niyonzima.
    Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amewapanga; Ally Mustafa 'Barthez', Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Deus Kaseke kuanza.
    Kwenye benchi wapo; Deo Munishi ‘Dida’, Benedicto Tinocco, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Pato Ngonyani, Said Juma ‘Makapu’, Salum Telela, Issoufou Boubacar, Matheo Anthony, Godfrey Mwashiuya, Malimi Busungu na Paul Nonga.
    Wachezaji wa Yanga SC wakifanya mazoezi mepesi kwenye Uwanja wenye madimbwi ya maji yaliyotokana na mvua
    Mpira umekwama kwenye maji, sheria zinasemaje? Mechi itachezwa?
    Mohammed Mpogolo akigawa jezi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo
    Kiungo mahiri, Mzimbabwe Thabani Kamusoko akiingia uwanjani
    Kiungo maridadi, Mnyarwanda Haruna Niyonzima akiingia uwanjani
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MVUA YATISHIA AMANI PAMBANO LA YANGA SC NA CERCLE JOACHIM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top