• HABARI MPYA

  Friday, February 12, 2016

  MUNTHALI AFUNGIWA MIEZI MIWILI KWA KUSAINI KLABU MBILI WAKATI MMOJA

  BEKI wa Zambia, Christopher Munthali (pichani kushoto) amefungiwa miezi miwili kucheza soka kwa kuvunja kinyume cha utaratibu Mkataba wake na klabu yake, Power Dynamos.
  Kamati ya Hadhi za Wachezaji ya Chama cha Soka Zambia (FAZ), Februari 10 mwaka huu iliamua kuifariji Power baada ya mchezaji huyo kusaini Mkataba mwingine na Nkana Desemba mwaka jana, akidai ni mchezaji huru.
  Mkataba wa Munthali na Power unatarajiwa kumalizika Desemba 31, mwaka 2016, lakini Nkana ikadai ilimaini beki huyu kama mchezaji huru baada ya Mkataba wake na wapinzani wao, Kitwe kumalizika Desemba 31, mwaka 2015.
  "Christopher Munthali amefungiwa kwa miezi miwili kujihusisha na soka," amesema Msemaji wa FAZ, Nkweto Tembwe.
  Kifungo hicho kinahusisha majukumu yake ya Chipolopolona inamaanisha Munthali atakosa mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 dhidi ya Kongo-Brazzaville utakaofanyika Machi 23 nyumbani na Machi 27.
  Munthali pia ameagizwa kurejea Power ambao walikuwa wamemtoa kwa mkopo Nkana msimu wa mwaka 2013 na 2014, baada ya baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
  Wakati huo huo, Nkana imepigwa faini ya dola za Kimarekani 1000.00 kwa kuhusika na udanganyifu huo.
  “Nkana wamepigwa faini ya wacha K10, 000.00 (dola1000.00) kwa kushindwa kufuata taratibu wakati wa kumsajili Munthali ambaye alikuwa ana Mkataba na Power Dynamos,” amesema Tembwe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUNTHALI AFUNGIWA MIEZI MIWILI KWA KUSAINI KLABU MBILI WAKATI MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top