• HABARI MPYA

  Thursday, February 04, 2016

  MBEYA CITY YAZINDUKA YAILAZA JKT RUBU 2-1 KARUME

  TIMU ya Mbeya City imezinduka baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu mchana wa leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Ushindi huo, unaifanya timu hiyo ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kufikisha pointi 17 baada ya kucheza mechi 17 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 10, wakiishusha Kagera Sugar yenye pointi 15 za mechi 17 pia. 
  Kikois cha Mbeya City kilichoifunga 2-1 JKT Ruvu leo Karume

  Katika mchezo wa leo, Mbeya City walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 23 kupitia kwa Hassan Mwasapili aliyemalizia pasi ya Ramadhani Chombo ‘Redondo’ ambaye naye alipata pasi ya Haruna Moshi ‘Boban’.
  JKT Ruvu ilisawazisha bao hilo dakika ya 38 kupitia kwa Mussa Juma aliyefumua shuti kali baada ya kupata pasi ya kiungo wa zamani wa Yanga SC, Hassan Dilunga.
  Yohanna Morris aliifungia Mbeya City bao la pili dakika ya 45 akiunganisha kwa shuti kali kona maridadi iliyochongwa na Mwasapili.
  Kipindi cha pili, JKT Ruvu walijizatiti na kusaka kwa juhudi bao la kusawazisha bila mafanikio kutokana na umakini na uimara wa Mbeya City leo.
  Kikosi cha JKT Ruvu kilikuwa: Shaaban Dihile, Michael Aidan, Paul Mhidze, Nurdin Mohammed, Issa Ngao/Nashon Naftali dk56, Madenge Ramadhani, Hamisi Thabit/Amos Edward dk46, Hassan Dilunga, Gaudence Mwaikimba, Mussa Juma na Emmanuel Pius/Najim Magulu dk64. 
  Mbeya City; Hanington Kalyesebula, John Banda, Hassan Mwasapili, Yohana Morris/Tumba Swedi dk83, Deogratius Julius, Kenny Ally, Joseph Mahundi/Themi Felix dk70, Raphael Alpha, Ditrim Nchimbi, Haruna Moshi ‘Boban’ na Ramadhani Chombo ‘Redondo’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAZINDUKA YAILAZA JKT RUBU 2-1 KARUME Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top