• HABARI MPYA

    Tuesday, February 02, 2016

    MANJI ‘AMTUMA’ MAKAMU WAKE KWENDA KUSHUGHULIKIA POINTI TATU MBEYA

    RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
    Febaruri 3, 2016 
    Prisons Vs Yanga SC
    Simba SC Vs Mgambo JKT
    Kagera Sugar Vs Majimaji
    JKT Ruvu Vs Mbeya City
    African Sports vs Mwadui FC
    Mtibwa Sugar Vs Toto Africans
    Feburari 4, 2016
    Coastal Union Vs Ndanda FC
    Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji (kulia) amemuagiza Makamu wake, Clement Sanga (kushoto) kwenda kushughulikia pointi tatu kesho Mbeya

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    BAADA ya kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Coastal Union, Yanga SC imejizatiti zaidi kuelekea mchezo wake wa kesho na Prisons.
    Yanga SC ililala 2-0 mbele ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kesho inashuka Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kuwavaa Prisons.
    Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji amemuagiza Makamu wake, Clement Sanga kwenda Mbeya kuhakikisha timu inashinda kesho.
    Na Sanga ameondoka leo Dar es Salaam na timu ya watu wa Kamati ya Mashindano, chini ya Mwenyekiti Isaac Chanji kuipigania timu ishinde kesho.
    Na sababu ya kupeleka viongozi wake wakuu Mbeya ni baada ya kugundua mchezo uliopita dhidi ya Coastal kulikuwa kuna mapungufu ya nje ya Uwanja yaliyochangia timu kupoteza pointi zote tatu.
    Matokeo hayo yanaiweka pagumu Yanga SC katika harakati za kutetea ubingwa wake, ikibaki na pointi zake 39, baada ya kucheza mechi 16, wakati Azam FC iliyocheza mechi 15 ina pointi 39 pia, huku Simba wakiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 16.
    Kwa ujumla, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho na mbali na Prisons kuikaribisha Yanga SC, Simba SC watakuwa wenyeji wa Mgambo JKT Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Uwanja wa Kambarage, Shinyanga – Kagera Sugar wataikaribisha Majimaji, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Mbeya City, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga African Sports wataikaribisha Mwadui FC wakati Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Toto Africans Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    Alhamisi Ligi Kuu itaendelea kwa mchezo mmoja tu kati ya Coastal Union na Ndanda FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI ‘AMTUMA’ MAKAMU WAKE KWENDA KUSHUGHULIKIA POINTI TATU MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top