• HABARI MPYA

    Tuesday, February 02, 2016

    MALINZI 'AMPA TANO' RAIS MSTAAFU DK KIKWETE KUKUBALI UTEUZI WA CAF

    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanznaia (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete kwa kukubali uteuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirika la Huduma za Afya kwa Jamii (GAVI) utakaomfanya kuwa balozi wa chanjo za mradi huo Afrika na duniani.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) amempongeza Rais mstaafu, Jakay Kikwete kwa kuteuliwa na CAF na GAVI kuwa balozi wa maradi wa chanjo

    “Familia ya mpira wa miguu inajua umuhimu wa chanjo na hasa katika maendeleo ya vipaji na wanamichezo kwa ujumla na jinisi chanjo inavyoweza kuwapa watoto siyo tu fursa ya maendeleo bali pia haki ya kuishi” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
    Katika barua hiyo, Malinzi ameelezea furaha ya TFF kuona kiongozi wa Tanzania akiongoza mapambano ya kuokoa afya na uhai wa kizazi cha sasa na kijacho katika Afrika na dunia kwa ujumla.
    “TFF itaunga mkono juhudi zako ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na ushirika wa chanjo” ilimalizia barua hiyo ambayo nakala yake imetumwa kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI 'AMPA TANO' RAIS MSTAAFU DK KIKWETE KUKUBALI UTEUZI WA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top