• HABARI MPYA

  Thursday, February 04, 2016

  MALI YATINGA FAINALI CHAN, KUIVAA DRC JUMAPILI AMAHORO

  TIMU ya taifa ya Mali imefanikiwa kuingia Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya ivory Coast leo mjini Kigali, Rwanda.
  Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Yves Bissouma dakika ya 88, baada ya kuingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Sekou Koita kipindi cha pili.
  Bossouma alifunga bao zuri, kwani baada ya kupokea pasi ya Hamidou Sinayoko akamtoka Badra Ali Sangare na kutumbukiza mpira nyavuni.

  Sasa Mali itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika fainali Februari 7 kuanzia Saa 12:30 Uwanja wa Amahoro, wakati Ivory Coast itamenyana na Guinea kuwania nafasi ya tatu Uwanja huo huo kuanzia Saa 9:00 Alasiri.
  DRC ilitinga Fainali baada ya kuifunga Guinea kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Amahoro pia.
  Ikumbukwe hizi ni Fainali za nne za CHAN, baada ya ziIe za mwaka 2009 Ivory Coast, 2011 Sudan na 2014 Afrika Kusini ambako Libya waliibuka mabingwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALI YATINGA FAINALI CHAN, KUIVAA DRC JUMAPILI AMAHORO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top