• HABARI MPYA

  Saturday, February 13, 2016

  JKU YASONGA MBELE BILA JASHO KOMBE LA CAF, MAFUNZO NA AS VITA LEO

  JKU ya Zanzibar (pichani juu) imefuzu bila jasho Raundi ya Awali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, kufuatia wapinzani wao, Gaborone United ya Botswana kujitoa kwenye michuano hiyo.
  Msemaji wa Chama cha Soka Zanzibar, Ally Cheupe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba mchezo kati ya JKU na Gaborone United uliokuwa ufanyike kesho kuanzia Saa 10:30 jioni Uwanja wa Amaan, Zanzibar sasa hautakuwepo.
  Cheupe amesema hiyo inafuatia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutuma taarifa ZFA juu ya kujitoa kwa Gaborone United.
  Sasa JKU inasonga mbele Raundi ya kwanza ya michuano hiyo, ambako itamenyana na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda na Khartoum III ya Sudan.
  Wawakilishi wengine wa Zanzibar kwenye michuano ya Afrika, Mafunzo FC leo wanatarajiwa kumenyana na A.S Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuanzia saa 10:30 jioni Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKU YASONGA MBELE BILA JASHO KOMBE LA CAF, MAFUNZO NA AS VITA LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top