• HABARI MPYA

  Tuesday, February 16, 2016

  HAWA NDIYO WATAKAOCHEZESHA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI TAIFA, KATIKATI ‘MDADA’

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  REFA wa kike, Jonesia Rukyaa wa Kagera ndiye anatarajiwa kupuliza kipyenga katika mchezo wa watani wa watani wa jadi, Simba na Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Rukyaa aliyechezesha pambano la mwisho la Nani Mtani Jembe Simba SC ikiifunga Yanga SC 2-0 mwaka juzi mabao ya Awadh Juma na Elias Maguri kwa mara ya pili katika historia yake atachezesha mechi ya watani Jumamosi.
  Jonesia Rukyaa wa pili kushoto kabla ya pambano la mwisho la Nani Mtani Jembe

  Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Rukyaa refa asiye na mzaha kabisa uwanjani, atasaidiwa na Josephat Burali wa Tanga na Samuel Mpenzu wa Arsusha.
  Refa wa akiba atakuwa Elly Sasii wa Dar es Salaam, wakati Kamisaa atakuwa mshambuliaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza, Khalid Bitebo ‘Zembwela’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAWA NDIYO WATAKAOCHEZESHA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI TAIFA, KATIKATI ‘MDADA’ Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top