• HABARI MPYA

  Monday, February 15, 2016

  DOMAYO: MIMI KUONDOKA AZAM FC NI UKOSEFU WA FADHILA

  Na Mwandishi Wetu, TANGA
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Frank Raymond Domayo amesema kwamba Aprili 29, mwaka huu anamaliza Mkataba wake katika klabu ya Azam FC, lakini ‘moyo mzito’ kuhamia klabu nyingine hata akipewa Mlima Kilimanjaro.
  Kwa nini? Domayo anajibu; “Hii klabu imenifanyia wema sana, imeokoa maisha yangu ya soka. Kama siyo Azam sidhani kama leo ningekuwa nacheza soka,”amesema.
  Domayo alijiunga na Azam FC mwaka juzi, akitokea Yanga SC ya Dar es Salaam pia, lakini wakati wa kufanyiwa vipimo vya afya ikagundulika alikuwa anacheza msuli wake mmoja wa paja ukiwa umechanika.
  Frank Domayo baada ya kufanyiwa upasuaji mwaka juzi 

  Azam FC ikampandisha ndege hadi Afrika Kusini kwenda kwa mtaalamu kufanyiwa upasuaji wa kina na kuwa nje ya Uwanja kwa msimu mzima akitoka tu kusaini Mkataba wa miaka miwili na timu ya bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake.
  Na baada ya mwaka mzima wa kuwa nje, msimu huu Domayo ameanza taratibu kurejea katika kiwango chake wakati na Mkataba wake unaelekea ukingoni. “Sina tatizo na Azam FC, hii timu imenifanyia wema sana, hatujakaa mezani kuzungumzia Mkataba mpya, lakini naamini hakuna kitakachoshindikana,”amesema.
  Domayo amesema kwa wema ambao Azam FC walimfanyia moyo wake ni mzito kuihama klabu hiyo, hata itokee klabu nyingine ya kumpa ofa kubwa zaidi. “Naona sasa ni wakati wa kulipa fadhila Azam, wamenifanyia wema sana, sitarajii kuondoka hata itokee klabu ya kunipa nini, mimi nitabaki Azam FC,”amesema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DOMAYO: MIMI KUONDOKA AZAM FC NI UKOSEFU WA FADHILA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top