• HABARI MPYA

  Sunday, February 14, 2016

  COASTAL UNION YAICHAPA AZAM FC 1-0 MKWAKWANI, MAKOSA YA AISHI YAIGHARIMU TIMU

  Na Mwandishi Wetu, TANGA
  AZAM FC imeshindwa kuiengua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC, baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
  Shukrani zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee, ambalo linavunja rekodi ya Azam FC kutofungwa msimu huu, beki wa kulia Miraj Adam aliyetikisa nyavu za timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake dakika ya 67.
  Adam aliyefunga pia katika ushindi wa 2-0 Coastal Union ikivunja rekodi ya Yanga SC kutofungwa msimu huu – leo alifunga kwa shuti la mpira wa adhabu pia, baada ya kuanzishiwa na beki mwenzake wa pembeni, Adeyum Saleh Ahmed.
  Shuti la Miraj Adam liliupenya ukuta wa Azam FC na kutinga nyavuni kuipa ushindi Coastal

  Kipa Aishi Manula ana kila sababu ya kubeba lawama kwa bao hilo, kwani alidaka mpira na kulala nao kwa muda mrefu huku akiugulia maumivu badala ya kuutoa nje kwanza na refa
   Vincent Mlabu kutoka Morogoro aliyesaidiwa na Gasper Ketto na Mohammed Mkono akawaadhibu Azam.
  Matokeo hayo yanaifanya Coastal Union ifikishe pointi 16 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda hadi nafasi ya 13, kutoka ya 16 ilipokuwa inashikilia mkia, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 42 za mechi 17, nyuma ya Yanga SC yenye pointi 43 za mechi 18 na Simba SC pointi 45 za mechi 19.
  Kikosi cha Coastal Union kilikuwa; Fikirini Bakari, Hamad Juma, Adeyum Saleh Ahmed, Mbwana Hamisi ‘Kibacha’, Miraj Adam, Sabo Youssouf, Juma Mahadhi, Abdulhalim Humud, Abasarim Chidiebere, Ally Ahmed ‘Shiboli’/Ayoub Yahya dk78 na Nassor Kapama.
  Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Said Mourad, Serge Wawa, Farid Malik/Gardiel Michael dk46, Michael Balou, Frank Domayo/Salum Abubakar dk46, Jean Mugiraneza, John Bocco na Allan Wanga/Kipre Tchetche dk69.
  Wachezaji wa Coastal Union wakishangilia bao lao lao
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA AZAM FC 1-0 MKWAKWANI, MAKOSA YA AISHI YAIGHARIMU TIMU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top