• HABARI MPYA

  Monday, February 15, 2016

  BUSUNGU: HAKUNA BEKI WA KUNINYIMA USINGIZI SIMBA SC

  Na Mwandishi Wetu, PEMBA
  MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Malimi Busungu amesema mabeki wa Simba SC ni wa kawaida na wanapitika, kikubwa ni mipango tu.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo kisiwani Pemba, ambako timu yake imeweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao hao, Busungu aliye katika msimu wake wa kwanza Yanga SC amesema kwamba hakuna beki wa kumnyima raha Simba SC.
  “Mabeki wa Simba SC ni wa kawaida sana tu na wanapitika, kikubwa ni mipango tu,”amesema Busungu kuelekea mchezo wa mahasimu wa jadi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Malimi Busungu amesema hakuna beki wa kumnyima raha Simba SC

  Alipoulizwa kama atarudia kuwafunga Simba SC kama alivyofanya katika mchezo wa kwanza, Busungu alisema; “Kikubwa ni timu kushinda siyo nani kufunga, kwani unategemea kama nitapata nafasi nitawaacha?”alisema Busungu ambaye alifunga bao moja katika ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza mwaka jana.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mgambo JKT, amesema mechi dhidi ya Simba inatarajiwa kuwa ngumu kwa sababu wapinzani wao pia wana timu nzuri.
  “Na pia sisi tuna mapungufu yetu, na wao wana mapungufu yao, inategemea nani atatumia vizuri makosa ya mwenzake, ila sisi tunajipanga vizuri kwa ajili ya kushinda hiyo mechi,”amesema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BUSUNGU: HAKUNA BEKI WA KUNINYIMA USINGIZI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top