• HABARI MPYA

  Thursday, February 11, 2016

  AZAM TV KUONYESHA LIVE MECHI ZA LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO

  MECHI ZA CAF ZITAKAZOONYESHWA LIVE AZAM TV;

  Ijumaa Februari 12, 2016
  Vipers SC v Enyimba SC
  Uwanja wa Mandela, Kampala, (Saa 10:00 Jioni)
  Chaneli; Azam Sports HD na AzamONE
  Jumamosi Februari 13, 2016
  Sports Club Villa v Alwatan Sudan
  Uwanja wa Mandela, (Saa 10:00 Jioni)
  Chaneli; AzamExtra
  Jumamosi Februari 13, 2016
  Mafunzo FC v A.S Vita
  Uwanja wa Amaan, Zanzibar (Saa 10:30 Jioni)
  Chaneli; ZBC 2
  Jumapili Februari 14, 2016
  JKU FC v Gaborone United
  Uwanja wa Amaan, (Saa 10:30 Jioni)
  Chaneli; ZBC 2
  Kikosi cha Mafunzo ambacho kitamenyana na A.S. Vita ya DRC Jumamosi Uwanja wa Amaan, Zanzibar

  TELEVISHENI ya Azam TV wikiendi hii itaonyesha mechi nne za michuano ya klabu ya Shirikisho la Soka Afrika, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho, zitakazozihusisha timu za Uganda na Zanzibar.
  Mechi hizo ni kati ya wenyeji Vipers FC dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika, Enyimba International FC ya Nigeria itakayochezwa kesho kuanzia saa 10:00 jioni Uwanja wa Mandela mjini Kampala, Uganda.
  Mchezo huo wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa utaonyeshwa Live kwenye chaneli ya Azam Sports HD na AzamONE.
  Azam TV wataonyesha pia mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Jumamosi kuanzia Saa 10:00 jioni kati ya wenyeji SC Villa dhidi ya Alwatan ya Sudan kupitia chaneli ya Azam Extra.
  Azam TV pia wataonyesha mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya wenyeji Mafunzo FC dhidi ya A.S Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jumamosi kuanzia saa 10:30 jioni Uwanja wa Amaan, Zanzibar kupitia chaneli ya ZBC 2.
  Azam TV itahitimisha mfululizo wa kuonyesha mechi za Ligi ya CAF Jumapili kwa kuonyesha mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya JKU FC na Gaborone United utakaochezwa Saa 10:30 jioni Uwanja wa Amaan, Zanzibar kupitia chaneli ya ZBC 2.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM TV KUONYESHA LIVE MECHI ZA LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top