• HABARI MPYA

  Wednesday, February 17, 2016

  ALIYEZIPA KOMBE LA AFRIKA ZAMBIA NA IVORY COAST ATUA MOROCCO

  MFARANSA, Renard, mwenye umri wa miaka 47, aliyeshinda Kombe la Mataifa ya Afrika mara mbili, kwanza akiwa na Zambia mwaka 2012 na baadaye akiwa na Ivory Coast mwaka jana, anachukua nafasi ya mzalendo, Badou Zaki.

  Herve Renard ameteuliwa kuwa kocha wa Morocco jana akirithi mikoba ya Badou Zaki aliyeondolewa wiki iliyopita

  Ndoa ya Zaki na Shirikisho la Soka Morocco (FRMF) ilivunjika kwa makubaliano ya pande zot mbili wiki iliyopita, baada ya miezi 20 ya kuwa kazini, kutokana na matokeo yasiyoridhisha.
  Renard aliweka wazi mipango katika timu ya taifa ya Morocco mara tu baada ya uteuzi huo.
  "Chaguo la kwanza ni, wazi kufuzu Fainali za Mataifa  ya Afrika mwaka 2017, siyo mbali sana, na kabla ya hapo ni kwamba kuna mwanzo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka 2018, hivyo ni ratiba muhimu mno,"amesema Mfaransa huyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALIYEZIPA KOMBE LA AFRIKA ZAMBIA NA IVORY COAST ATUA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top