• HABARI MPYA

    Thursday, January 07, 2016

    YANGA SC YAPEWA FRIENDS RANGERS KOMBE LA TFF, SIMBA NA BURKINA FASO, AZAM NA ASHANTI

    RATIBA RAUNDI YA TATU LA AZAM SHIRIKISHO…
    Januari 12, 2016
    Majimaji Vs JKT Mlale (Majimaji, Songea)
    Januari 23, 2016
    Pamba Vs Toto Africans (CCM Kirumba, Mwanza)
    Ndanda FC Vs Mshikamano (Nagwanda, Mtwara) Burkina Faso Vs Simba SC (Jamhuri, Morogoro)
    Januari 27, 2016
    Yanga SC Vs Friends Rangers (Taifa, Dar es Salaam) Njombe Mji Vs Prisons (Amani, Makambako) Stand Utd Vs Mwadui FC (Kambarage, Shinyanga)
    Kagera Sugar Vs Rhino Rangers (Mwinyi, Tabora)
    Panone Vs Madini (Uwanja utatajwa baadaye)
    Mtibwa Sugar Vs Abajalo (Turiani, Manungu)
    Lipuli/Kurugenzi Vs JKT Ruvu (Samora, Iringa)
    Ashanti United Vs Azam FC (Karume, Dar es Salaam)
    Africa Sports Vs Coastal Union (Mkwakwani, Tanga)
    Geita Gold Vs Mgambo Shooting (Geita)
    Singida United Vs Mvuvuma (Namfua, Singida)
    Wenda v Mbeya City (Uwanja utatajwa baadaye)
    Friends Rangers watamenyana na Yanga SC Raundi ya Tatu Kombe la TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa Bara, Yanga SC watamenyanana Friends Rangers katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup Januari 27, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema mzunguko wa tatu inatarajiwa kuendelea Januari 12 na wikiendi ya Januari 23-27 kwa timu 32 kuchuana kuwania kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
    Timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimeingia moja kwa moja mzunguko wa tatu ambapo sasa zinajumuika na timu 16 zilizofuzu kutoka raundi ya pili yenye timu kutoka ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili.
    Jumamosi, Januari 12, Majimaji itacheza dhidi ya JKT Mlale uwanja wa Majimaji mjini Songea, Januari 23 Pamba v Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba, Ndanda FC v Mshikamano Nagwanda Sijaona Mtara, huku Burkinafaso wakiwakaribisha Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
    Januari 24, Yanga SC watacheza na Friends Rangers uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Njombe Mji v Tanzania Prisons uwanja wa Amani Makambako, mjini Shinyanga Stand United watachuana dhidi ya Mwadui FC.
    Mechi zingine ni Kagera Sugar v Rhino Rangers, Panone v Madini, Mtibwa Sugar v Abajalo, Lipuli/Kurugenzi v JKT Ruvu, Ashanti United v Azam FC, Africa Sports v Coastal Union, Geita Gold v Mgambo Shooting, Singida United v Mvuvuma na Wenda v Mbeya City.
    Timu 15 zilizofuzu hatua ya tatu kutoka raundi ya pili ni Ashanti United, Pamba, Friends Rangers, Panone, Geita Gold, Mvuvuma, Burkinafaso, Rhino Rangers, Madini FC, JKT Mlale, Mshikamano FC, Njombe Mji, Wenda FC, Singida United, Abajalo huku mchezo mmoja kati ya Lipuli dhidi ya Kurugenzi ukichezwa leo hii kusaka timu ya kufuzu raundi ya tatu.
    Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika mwaka 2017.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAPEWA FRIENDS RANGERS KOMBE LA TFF, SIMBA NA BURKINA FASO, AZAM NA ASHANTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top