• HABARI MPYA

  Friday, January 15, 2016

  TFF YAMREJESHA KIM POULSEN, KUSAINI MKATABA WA KUFUNDISHA TENA NCHINI

  REKODI YA KIM POULSEN STARS
  Jumla ya Mechi; 18
  Mechi alizoshinda;          5
  Mechi alizofungwa;        7
  Mechi alizotoa sare;       6

  MECHI ZA TAIFA STARS CHINI YA KIM POULSEN;
  Mei 26, 2012
  Tanzania 0 – 0 Malawi (Kirafiki)
  Juni 2, 2012
  Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
  Juni 10, 2012
  Tanzania 2 – 1 Gambia (Kufuzu Kombe la Dunia)
  Juni 17, 2012
  Msumbiji 1 – 1 Tanzania (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
  Agosti 15, 2012
  Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)
  Novemba 14, 2012
  Tanzania 1-0 Kenya (Kirafiki)
  Desemba 22, 2012
  Tanzania 1-0 Zambia (Kirafiki)
  Januari 11, 2013
  Tanzania 1-2 Ethiopia (Kirafiki)
  Februari 6, 2013
  Tanzania 1-0 Cameroon (Kirafiki)
  Machi 24, 2013
  Tanzania 3-1 Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
  Juni 2, 2013
  Sudan 0 – 0 Tanzania (Mechi ya kirafiki Ethiopia)
  Juni 8, 2013 
  Morocco 2-1 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
  Juni 6, 2013 
  Tanzania 2-4 Ivory Coast (Kufuzu Kombe la Dunia)
  Julai 13, 2013
  Tanzania 0-1 Uganda (Kufuzu CHAN)
  Julai 27, 2013
  Uganda 3-1 Tanzania (Kufuzu CHAN)
  Septemba 7, 2013
  Gambia 2-0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
  Tanzania 0-0 Zimbabwe (Kirafiki Dar)
  Namibia 1-1 Tanzania (Kirafiki Windhoek)
  TFF ipo katika mchakato wa kusaini Mkataba na Kim Poulsen afundishe timu za vijana

  REKODI YA KIM KOMBE LA CECAFA CHALLENGE
  Jumla ya mechi alizocheza;   12
  Mechi alizoshinda; 5
  Mechi alizofungwa; 3
  Mechi alizotoa sare; 4

  MATOKEO YA KILIMANJARO STARS CHINI YA POULSEN;
  Novemba 25, 2012
  Tanzania  2–0  Sudan (Kundi B)
  Novemba 28, 2012
  Tanzania  0–1 Burundi (Kundi B)
  Desemba 1, 2012
  Tanzania 7-0 Somalia (Kundi B)
  Desemba 3, 2013
  Tanzania 2-0 Rwanda (Robo Fainali)
  Desemba 6, 2012
  Tanzania 0–3 Uganda (Nusu Fainali)
  Desemba 8, 2012
  Tanzania  1-1 Zanzibar (Zanzibar ikashinda penalti 6-5) 
  Novemba 28, 2013
  Tanzania 1-1  Zambia (Kundi B)
  Desemba 1, 2013
  Tanzania 1-0 Somalia (Kundi B)
  Desemba 4, 2013
  Tanzania 1-0   Burundi (Kundi B)
  Desemba 7, 2013
  Tanzania 2-2 Uganda (Robo Fainali, Stars ikashinda kwa penalti 3-2)
  Desemba 10, 2013
  Tanzania 0-1 Kenya (Nusu Fainali)
  Tanzania 1-1 Zambia (Mshindi wa tatu, Zambia wakashinda kwa penalti)

  Taifa Stars ya Kim Poulsen ilizifunga Cameroon, Morocco, Zambia na Gambia

  Na Mandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mdenmark, Kim Poulsen yupo nchini kukamilisha mipango ya Mkataba wa kufundisha timu za vijana za taifa.
  Kim, anarejea nchini baada ya mwaka mmoja na ushei tangu aondolewe kufundisha timu ya taifa ya wakubwa, Taifa Stars na nafasi yake kuchukuliwa na Mholanzi, Mart Nooij aliyeondolewa pia Agosti mwaka jana.
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56, alitua nchini kwa mara ya kwanza Aprili 2011 kufundisha timu za vijana kabla ya Mei 2012 kupandishwa Taifa Stars, kufuatia kuondolewa kwa Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen.
  Hata hivyo, mapema mwaka 2014 Kim aliondolewa Taifa Stars baada ya kumaliza Mkataba wake na kuajiriwa Mholanzi, Nooij huku Mdenmark huyo akienda Silkeborg IF ya kwao.
  Akiwa Taifa Stars, Kim alishinda mechi tano tu kati ya 18, huku akifungwa saba na kutoa sare sita,
  Mechi za kukumbukwa alizoshinda Kim ni dhidi ya Gambia 2-1 Kufuzu Kombe la Dunia, dhidi ya Zambia 1-0 kirafiki, dhidi ya Cameroon 1-0 kirafiki na dhidi ya Morocco 3-1 Kufuzu Kombe la Dunia.
  Kim aliiongoza timu ya Bara, Kilimanjaro Stars katika mechi 12 za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge, akishinda tano, sare nne na kufungwa tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAMREJESHA KIM POULSEN, KUSAINI MKATABA WA KUFUNDISHA TENA NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top