• HABARI MPYA

  Saturday, January 02, 2016

  SUNSHINE STARS YAGOMA KUUZA WACHEZAJI WAKE KWA KLABU ZA NIGERIA

  KLABU ya Sunshine Stars imeweka wazi kwamba haiko tayari kumuuza mchezaji yeyote kwa klabu pinzani ya Ligi Kuu ya Nigeria (NPFL).
  Wachezaji sita wa klabu hiyo ya Akure wanatakiwa na klabu mbalimbali na NPFL ambao ni Dayo Ojo, Seun Olulayo, Stephen Eze, Paul Onobi, kipa Ikechukwu Ezenwa na mfungaji wao bora wa msimu uliopita, Tunde Adeniji.
  Sunshine Stars imesema iko tayari kufanya biashara na klabu za nje tu juu ya wachezaji hao sita kwa matarajio ya kupata ofa nzuri.
  Wachezaji wa Sunshine Stars hawauzwi kwa klabu za Nigeria, huo ndiyo msimamo wa klabu 

  "Tunataka kuzungumza hii wazi kwamba hatuko tayari kumpoteza mchezaji wetu yeyote tegemeo. Tuko tayari kubaki nao na kuifanya timu iwe bora kuliko ilivyokuwa, huku tukipambana kuendeleza na kuongeza maslahi bora. 
  Tunaridhishwa na uwajibikaji wa wachezaji na tuna matumaini ya msimu bora," amesema Rais wa klabu, Akin Akinbobola, ambaye pia anawajibika kama Mwenyekiti wa klabu ya Ondo State Football Agency.
  "Hatuuzi kwa wapinzani wetu wa NPFL, lakini ikitokea ofa nzuri kutoka nje (ya Nigeria), tutaipokea na kuitafakari," ameongeza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SUNSHINE STARS YAGOMA KUUZA WACHEZAJI WAKE KWA KLABU ZA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top