• HABARI MPYA

    Wednesday, January 06, 2016

    SIMBA SC ‘YAANGUSHA MBUYU’, YAICHAPA 1-0 URA, MAMBO YA HAJIB HAYO!

    MAKUNDI, MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA MAPINDUZI 2016
    Kundi A: Simba SC, Jamhuri, JKU, URA
    Kundi B: Yanga SC, Mafunzo, Azam FC, Mtibwa Sugar
    (Mechi zote zitachezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar)

    Jan 3, 2016
    Yanga SC 3-0 Mafunzo
    Mtibwa Sugar 1-1 Azam FC (Saa 2:15 usiku)
    Jan 4, 2016
    JKU 1-3 URA (Saa 10:15 jioni)
    Simba SC 2-2 Jamhuri Saa 2:15 usiku)
    Jan 5, 2016
    Mafunzo 0-1 Mtibwa Sugar (Saa 10:15 jioni)
    Azam FC 1-1 Yanga SC (Saa 2:15 usiku)
    Jan 6, 2016
    Jamhuri 0-3 JKU (Saa 10:15 jioni)
    URA 0-1 Simba SC (Saa 2:15 usiku)
    Jan 7, 2016
    Azam Vs Mafunzo (Saa 10:15 jioni)
    Mtibwa Sugar Vs Yanga (Saa 2:15 usiku)
    Jan 8, 2016
    Jamhuri Vs URA (Saa 10:15 jioni)
    Simba SC Vs JKU (Saa 2:15 usiku)
    NUSU FAINALI
    Jan 10, 2016
    FAINALI
    Jan 13, 2016 (Saa 2:15 usiku)

    Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza mwenzao, Ibrahim Hajib (kulia) baada ya kufunga bao pekee leo

    Na Princess Asia, ZANZIBAR
    SIMBA SC imebisha hodi Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2016, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya URA ya Uganda katika mchezo wa Kundi A usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Shujaa wa Simba SC, alikuwa Ibrahim Hajib Migomba aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 
    37 kwa shuti lake la umbali wa mita 20, baada ya kupokea pasi ya beki Mrundi, Emery Nimubona.
    Simba SC inapanda kileleni mwa Kundi A baada ya kufikisha pointi nne, kutokana na mechi mbili, ikifuatiwa na URA yenye pointi tatu sawa na JKU, wakati Jamhuri wanashika mkia kwa pointi yao moja.
    Mshambuliaji wa Simba SC, Danny Lyanga akipambana na mabeki wa URA usiku wa leo

    Simba SC, mabingwa watetezi wa Kombe hilo, ilistahili ushindi katika mchezo wa leo, kutokana na kucheza kwa umakini na nidhamu ya hali ya juu, kiasi cha kuwadhibiti kabisa URA.
    Na ingeweza kutoka na ushindi mnene zaidi iwapo, washambuliaji wake wangetumia nafasi zaidi walizopata.
    Dakika ya 51, Danny Lyanga alimtoka vizuri Jimmy Kulaba, lakini shuti lake likatoka nje, wakati dakika ya 70, kipa wa URA, Brian Bwette alifanya kazi ya ziada kupangua mpira wa kichwa wa Mganda mwenzake, Hamisi Kizza aliyemalizia pasi ya Mwinyi Kazimoto
    Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B kuhitimishwa, Azam FC wakimenyana na Mafunzo, wakati Yanga SC watamenyana na Mtibwa Sugar usiku. 
    Simba SC itamaliza na JKU keshokutwa, wakati URA itamaliza na Jamhuri.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter Manyika, Emery Nimubona, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Brian Majwega dk64, Abdi Banda, Juuko Murushid, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Ibrahim Hajib/Awadh Juma dk83, Hamisi Kizza/Mussa Mgosi dk83 na Danny Lyanga.
    URA; Brian Bwette, Simeon Massa/Sharifin Kagimu dk47, Allan Munaaba, Jimmy Kulaba, Sam Senkoom, Oscar Agaba, Julius Ntambi, Said Kyeyune, Derrick Tekwo/Ronald Kigongo dk47, Villa Oromuchani na Elkanah Nkagwa/Peter Iwassa dk75. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC ‘YAANGUSHA MBUYU’, YAICHAPA 1-0 URA, MAMBO YA HAJIB HAYO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top