• HABARI MPYA

  Tuesday, January 05, 2016

  SAMATTA APAA KESHO KUFUATA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA, ATAPEWA ‘KAMPANI’ NA MWESIGWA WA TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine kesho Jumatano anatarajiwa kuongozana na mshambuliaji, Mbwana Ally Samatta kwenda Nigeria kwenye sherehe za tuzo za Wachezaji Bora Afrika 2015.
  Nyota huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, ameingia tatu bora ya Tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika pamoja na kipa Robert Kidiaba anayecheza naye TP Mazembe ya DRC na Baghdad Boundjah wa Algeria na Etoile du Sahel ya Tunisa.
  Mbwana Samatta akiicheza Tanzania katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Malawi mwaka jana

  Katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa Jumla wa Afrika, walioingia fainali ni Andre Ayew wa Ghana na Swansea City, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund na Yaya Toure wa Ivory Coast na Manchester City, anayeshikilia tuzo hiyo.
  Mwesigwa anatarajiwa kuondoka na Samatta kuelekea Nigeria katika mji wa Abuja ambapo sherehe za utoaji tuzo hizo zitafayika Alhamisi.
  Samatta anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo baada ya kuiwezesha Mazembe kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake manane.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi amemtakia kila la heri Samatta katika kinyanganyiro hicho cha uchezaji bora na kusema kwa niaba ya Watanzania wote wanamuombea dua njema aweze kushinda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA APAA KESHO KUFUATA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA, ATAPEWA ‘KAMPANI’ NA MWESIGWA WA TFF Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top