• HABARI MPYA

    Friday, January 08, 2016

    RAIS MAGUFULI, MALINZI WAMWAGIA PONGEZI SAMATTA, AREJEA USIKU WA MANANE LEO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli amempongeza mshambuliaji Mbwana Ally Samatta kwa kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.  
    Samatta ameshinda tuzo hiyo jana katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa mjini Abuja, Nigeria akiwagaragaza kipa wa DRC, Robert Kidiaba anayecheza naye TP Mazembe ya DRC aliyeshika nafasi ya pili na Bounedjah Baghdad wa Etoile du Sahel na Algeria, aliyeshika nafasi ya tatu.
    Mbwana Samatta (kushoto) akiwa na Pierre Aubameyang wa Gabin aliyeshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika jana mjini Abuja

    Rais Magufuli aliye katika mwaka wake wa kwanza tangu aingie Ikulu kwa tiketi ya CCM kuchukua nafasi ya Dk Jakaya Mrishon Kikwete, amesema tuzo imempa heshima Mbwana binafsi, wachezaji wa Tanzania na taifa kwa ujumla.
    Aisha, naye Rais Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani.
    Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza Afrika baada ya kwashinda Robert Kidiaba (Congo DR) alieshika nafasi ya pili na Bounedjah Baghdad (Algeria) aliyeshika nafasi ya tatu.
    Kwa kushinda tuzo hiyo, Samatta amekua mchezaji wa kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kushinda tuzo kubwa barani Afrika.
    Pamoja na kushinda tuzo hiyo, Samatta pia amejumuishwa katika kikosi bora cha wachezaji wa Afrika kwa mwaka 2015 sambamba na Robert Kidiaba (Congo DR), Sergie Aurier (Ivory Coast), Aymen Abdenmor (Tunisia), Mohamed Meftah (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Yaya Toure (Ivory Coast), Yacine Ibrahim (Algeria), Andrew Ayew (Ghana), Mbwana Samatta (Tanzania), Pierre-Emercik Aubameyang (Gabon) na Baghdad Bounedjah (Algeria).
    Mshambuliaji Mbwana Samatta alieyambatana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine wanatarajia kuwasili nchini leo saa 8 usiku kwa shirika la ndege la Ethiopia.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS MAGUFULI, MALINZI WAMWAGIA PONGEZI SAMATTA, AREJEA USIKU WA MANANE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top