• HABARI MPYA

  Sunday, January 10, 2016

  MGANDA AWA KOCHA MPYA MSAIDIZI SIMBA SC, NI JACKSON MAYANJA

  MGANDA, Jackson Mayanja ameteuliwa kuwa Kocha Msaidizi wa Simba SC, kufuatia kuondoka kwa Suleiman Matola miezi miwili iliyopita.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba Mayanja aliyekuwa anaifundisha Coastal Union ya Tanga atajiunga na timu mara moja visiwani Zanzibar kuanza kazi, chini ya Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan Kerr kama.
  Kocha huyo wa zamani wa Kagera Sugar anatarajiwa kusaini Mkataba wa mwaka mmoja na Simba SC wenye kipengele cha kuongezewa, iwapo kazi yake itawaridhisha wenye timu.
  Jackson Mayanja sasa ndiye kocha mpya Msaidizi SImba SC

  "Ni mchakato ambao ulifanyika kwa uwazi na kwa kufuata taratibu na weledi mkubwa katika kutafuta mtu sahihi kwa kazi hiyo, na Uongozi pamoja na benchi zima la ufundi limeafikia kwa pamoja kumpatia mkataba kocha Mayanja kuwa kocha msaidizi wa Kikosi cha Simba" amesema Haji Manara.
  Kwa sasa kikosi cha Simba SC kipo visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi na leo kitamenyana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MGANDA AWA KOCHA MPYA MSAIDIZI SIMBA SC, NI JACKSON MAYANJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top