• HABARI MPYA

  Thursday, January 14, 2016

  CHANONGO MAMBO SAFI MAZEMBE, ASUBIRIWA MOISE KATUMBI TU AMALIZE MPANGO

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wawili wa Stand United, beki Abuu Ubwa na kiungo Haroun Chanongo wanatarajiwa kurejea usiku wa leo kutoka Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya 
  Kongo (DRC).
  Wawili hao walikuwa Lubumbashi kwa ajili ya kufanya majaribio katika klabu ya TP Mazembe ya huko na baada ya wiki moja wanarejea nyumbani.
  Meneja wa wachezaji hao, Jamal Kisongo ambaye pia ni Meneja wa mshambuliaji Mbwana Samatta ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba taarifa za awali kuhusu majaribio ya vijana hao ni nzuri.
  Hata hivyo, Kisongo amesema kwamba majibu rasmi wanatarajia kuyapata baada ya Rais wa Mazembe, Moise Katumbi kutoa uamuzi.
  Chanongo (kushoto) na Ubwa (kulia) walipokuwa majaribio TP Mazembe. Wanatarajiwakurejea usiku wa leo

  “Ni kwamba majibu ya awali ni mazuri, lakini nitalazimika kusubiri taarifa rasmi baada ya bosi mwenyewe (Moise Katumbi) ambaye kwa sasa yupo Ulaya kurejea na kuamua baada ya kupewa ripoti,”amesema Kisongo.
  Baada ya kuonja matunda ya washambuliaji wawili wa Kitanzania, Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wapo Lubumbashi kwa mwaka wa nne sasa, Mazembe imefungua milango zaidi kwa wachezaji wa Tanzania.
  Huku ikiwa katika mpango wa kuwauza wawili Ulaya hao baada ya miaka minne ya mafanikio, Mazembe iliwapa nafasi ya majaribio Chanongo na Ubwa ambao kwa mujibu wa Kisongo, taarifa za awali zinasema wamefanya vizuri.
  Na sasa anasubiriwa mtu wa maamuzi, Moise Katumbi aamue mustakabali wa vijana hao.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHANONGO MAMBO SAFI MAZEMBE, ASUBIRIWA MOISE KATUMBI TU AMALIZE MPANGO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top