• HABARI MPYA

    Sunday, January 03, 2016

    BINGWA WA 10 KOMBE LA MAPINDUZI AANZA KUSAKWA LEO...YANGA NA MAFUNZO, MTIBWA NA AZAM

    ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
    Mwaka    Bingwa Mshindi wa Pili
    2007 Yanga SC Mtibwa Sugar 
    2008 Simba SC Mtibwa Sugar
    2009 Miembeni         KMKM
    2010 Mtibwa Sugar Ocean View
    2011 Simba SC   Yanga SC
    2012 Azam FC         Simba SC
    2013 Azam FC   Tusker FC
    2014 KCCA       Simba SC
    2015 Simba SC Mtibwa Sugar
    Wachezaji wa Yanga SC, Thabani Kamusoko (kushoto) na Mwinyi Hajji Mngwali (kulia) wakifanya mazoezi na timu yao jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar kujiandaa na mchezo wa leo

    Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
    MICHUANO ya 10 ya Kombe la Mapinduzi, inatarajiwa kuanza leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar mabingwa wa zamani, Yanga SC wakimenyana na wenyeji Mafunzo FC kuanzia Saa 10:15 jioni.
    Huo utakuwa mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo, kabla ya mabingwa wengine wa zamani wa Kombe la Mapinduzi, Mtibwa Sugar kucheza na Azam FC.
    Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Masoud Attai aliiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jana mchana kwamba maandalizi ya mashindano haya yamekamilika na wanatarajia mwaka huu michuano kuwa na ushindani zaidi.
    Alizitaja timu nane zitakazochuana kuwania ubingwa huo kuwa ni pamoja na mabingwa watetezi Simba SC, Yanga, Azam zote kutoka jijini Dar es Salaam, Mtibwa Sugar (Morogoro), Jamhuri, JKU, Mafunzo (Zanzibar) na URA ya Uganda.
    "Licha ya kuwa na timu chache, nawaahidi wadau wa soka wa Zanzibar na wageni wanaofika kushuhudia michuano hiyo kutoka nje ya Visiwa hivi kujiandaa kuona burudani nzuri na soka lenye ushindani kuanzia mechi za makundi hadi hatua ya fainali," alisema kiongozi huyo.
    Alisema kwamba kabla ya kufikia maamuzi ya kupunguza timu, walizingatia ubora na hadhi ya mashindano kuongezeka na baada ya kujiridhisha ndipo walifanya maamuzi.
    Alitaja zawadi za mashindano kwamba bingwa atapata Sh. Milioni 10 na mshindi wa pili atajinyakuliwa Sh. Milioni 5.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BINGWA WA 10 KOMBE LA MAPINDUZI AANZA KUSAKWA LEO...YANGA NA MAFUNZO, MTIBWA NA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top