• HABARI MPYA

  Thursday, January 07, 2016

  AZAM FC KUTETEA KOMBE LA KAGAME ZANZIBAR, CECAFA YAJA KIVINGINE 2016

  Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombr la Kagame, inatarajiwa kufanyika kati ya Julai na Agosti mwaka huu kisiwani Zanzibar.
  Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, (CECAFA), Nicholaus Musonye amesema pamoja na michuano hiyo kufanyika Zanzibar mwaka huu, pia wamejipanga kuendesha michuano ya U17 itakayofanyika Mei nchini Uganda, michuano ya Mpira wa miguu wa Wanawake (Uganda), Mashindano ya vijana chini ya miaka 20 (Burundi) huku michuano ya CECAFA Senior Challenge ikipangwa kufanyika nchini Sudan.
  Azam FC ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame

  Mwishoni mwa wiki uongozi wa Kamati ya Utendaji wa CECAFA ulikutana nchini Sudan na kufanya kikao chake cha kwanza chini ya Rais Dkt Mutasim Ghafar amabye pia ni Rais wa Chama cha Soka nchini Sudani (SFA).
  Katika kikao hicho, CECAFA ilitangaza kumpa Leodgar Tenga Rais wa heshima wa Cecafa huku pia wakisaini makubaliano ya uendelezaji wa soka la vijana na Chama cha Soka cha Saudi Arabia (SAFF) kupitia kwa Rais wake Ahmed Alharbi.
  Ikumbukwe Azam FC ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame ambao walilitwaa mwaka jana Dar es Salaam kwa kuwafunga Gor Mahia ya Kenya katika fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC KUTETEA KOMBE LA KAGAME ZANZIBAR, CECAFA YAJA KIVINGINE 2016 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top