• HABARI MPYA

  Sunday, January 03, 2016

  ARSENAL YATANUA KWAPA KILELENI ENGLAND, MAN UNITED YAFUTA GUNDU

  MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND JANA
  Watford 1-2 Manchester City
  Norwich City 1-0 Southampton
  Leicester City 0-0 Bournemouth
  Arsenal 1-0 Newcastle United
  Manchester United 2-1 Swansea City
  West Bromwich Albion 2-1 Stoke City
  Sunderland 3-1 Aston Villa
  West Ham United 2-0 Liverpool
  Beki Laurent Koscielny akishangilia baada ya kuifungia baio pekee Arsenal jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  TIMU ya Arsenal imekaa sawa kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushndi wa bao 1-0 jana dhidi Newcastle United Uwanja wa Emirates.
  Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee, Laurent Koscielny dakika ya 72 na sasa timu ya Arsene Wenger inafikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 20, ikifuatiawa na Leicester City pointi 40 za mechi 20 pia, Manchester City pointi 39 za mechi 20 na Tottenham Hotspur pointi 35 baada ya kucheza mechi 20 pia.
  Manchester United imefuta mikosi jana baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea City Uwanja wa Old Trafford, mabao yake yakifungwa na Anthony Martial dakika ya 47 na Nahodha Wayne Rooney dakika ya 77, huku  Gylfi Sigurdsson akiwafungia wageni dakika ya 70.
  Yaya Toure akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  United sasa inafikisha pointi 33 baada ya kucheza mechi 20 na kuendelea kukamata nafasi ya tano.
  Manchester City imepata ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya Watford Uwanja wa Vicarage Road.
  Aleksandar Kolarov alianza kujifunga dakika ya 55 kuwapatia Watford bao la kuongoza kabla ya Gnegneri Yaya Toure kuwasawazishia City dakika ya 82 na Sergio Aguero kufunga la pili dakika ya 84.
  Liverpool imegongwa 2-0 na West Ham United Uwanja wa Boleyn Ground mabao ya Michail Antonio dakika ya 10 na Andy Carroll dakika ya 55, wakati Norwich City imeilaza 1-0 Southampton bao pekee la Alexander Tettey dakika ya 76 Uwanja wa Carrow Road.
  Nahodha Wayne Rooney (katikati) akipongezwa na wenzake Anthony Martial na Bastian Schweinsteiger baada ya kuifungia Man United bao la ushindi jana  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Leicester City imelazimishwa sare ya 0-0 na Bournemouth Uwanja wa King Power, wakati West Bromwich Albion imeichapa 2-1 Stoke City Uwanja wa The Hawthorns, mabao yake yakifungwa na Stephane Sessegnon dakikia ya 60 na Jonny Evans dakika ya 93, huku la wageni likifungwa na Jonathan Walters dakika ya 81.
  Sunderland imeichapa 3-1 Aston Villa mabao yake yakifungwa na Patrick van Aanholt dakika ya 30,  Jermain Defoe dakika ya 72 na 92, huku la Villa likifungwa na Carles Gil de Pareja Vicent dakika ya 63 Uwanja wa Light.
  Mshambuliaji wa West Ham, Andy Carroll akipongezwa na mchezaji mwenzake, Mark Noble baada ya kufunga jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YATANUA KWAPA KILELENI ENGLAND, MAN UNITED YAFUTA GUNDU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top