• HABARI MPYA

    Saturday, August 01, 2015

    USAJILI LIGI KUU BADO WIKI MOJA KUFUNGWA, SIMBA WASOTEA SAINI YA MAVUGO, YANGA…

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    DIRISHA la Usajili kwa klabu za Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (RCL) linatarajiwa kufungwa tarehe 06 Agosti, 2015.
    Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linavikumbusha vilabu vyote kufanya usajili wa wachezaji wao mapema kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo, ili kuondokana na usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho.
    Pindi dirisha hilo litakapofungwa Agosti 06, hakuna klabu au timu yoyote itakayoweza kufanya tena usajili wake, hivyo ni vyema vilabu vitahakikisha vinamaliza mausala ya usajili mapema kabla ya siku ya mwisho.
    Simba SC inasotea uhamisho wa Laudit Mavugo kutoka Vital'O

    Wakati ikiwa imebaki wiki moja usajili kufungwa, Simba SC inahangaika kumalizana na klabu ya Vital’O ya Burundi juu ya mshambuliaji Laudit Mavugo ambaye tayari imemsainisha Mkataba wa miaka miwili.
    Watani wao Yanga SC, nao wanataka kuboresha kikosi chao cha baada ya kutolewa Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: USAJILI LIGI KUU BADO WIKI MOJA KUFUNGWA, SIMBA WASOTEA SAINI YA MAVUGO, YANGA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top