• HABARI MPYA

    Tuesday, September 03, 2013

    IRINGA YAINYANYASA RUVUMA COPA COCA-COLA

    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA SEPTEMBA 3, 2013, SAA  11:52 JIONI
    IRINGA imeanza kwa kishindo michuano ya Copa Coca-Cola kwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Septemba 3 mwaka huu) kuitandika Ruvuma mabao 4-0.
    Hadi mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa dakika ya 14 na Justin Luvanda huku Alphonce Kalinga akifunga la pili dakika ya 43.
    Mabao mengine yalifungwa na Juma Rogani katika dakika ya 49 na Luvanda akafumania tena nyavu dakika ya 59.
    Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa Ruvuma kupoteza ambapo ya kwanza ililala mbele ya wenyeji Mbeya kwa mabao 3-0.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: IRINGA YAINYANYASA RUVUMA COPA COCA-COLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top