• HABARI MPYA

  Wednesday, June 06, 2012

  BREAKING NEWS;YONDAN AKAMILISHA USAJILI YANGA NA KUKANA KUSAINI SIMBA

  Yondan akikamilisha usajili wake Yanga, mbele ya Seif Magari kulia leo usiku, Kushoto ni mtu wa Simba, ambaye alimpeleka mchezaji huyo kumaliza usajili naye akapewa posho yake.
  KELVIN Patrick Yondan, beki wa kati wa Simba amekana kusaini mkataba wowote na Simba na amesema yeye amesaini Yanga tu mkataba wa miaka miwili.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY usiku huu, Yondan amesema Simba wanampakazia kusaini mkataba mpya na anataka wapenzi wote wa soka Tanzania watambue kwamba kuanzia sasa yeye ni mchezaji halali wa Yanga.
  "Kesho tutaongea vizuri, nimechoka,"alisema Yondan baada ya kukamilisha usajili wake, mbele ya mgombea Ujumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb na swahiba wake Seif Ahmad 'Magari' usiku huu.
  "Alikuwa amesaini kila kitu, kuna sehemu alikuwa hajamaliza kujaza leo, ndio amemalizia na ametuhakikishia hana mkataba na Simba, hivyo huyu ni mchezaji ambaye mimi na Seif tunamsajili kwa ajili ya klabu yetu kipenzi, Yanga,"alisema Bin Kleb.
  Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata ni kwamba, Yondan aliikana Yanga awali kwa sababu walimsainisha fomu bila kumpa fedha, lakini leo amepewa Milioni 30 zake taslimu na amemaliza kila kitu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BREAKING NEWS;YONDAN AKAMILISHA USAJILI YANGA NA KUKANA KUSAINI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top